• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ronaldo atoa kali kwa kusimamia vidole ili aonekane mrefu

    (GMT+08:00) 2014-11-07 10:08:23

    Vituko katu haviishi duniani, kwani mchezaji bora wa dunia kwa sasa Cristiano Ronaldo ametoa kali baada ya kuonekana akisimamia vidole vya mbele ili aonekane mrefu kuwazidi wenzie wakati wa kupiga picha. Ronaldo ameonekana akifanya hivyo kwenye mechi ya Real Madrid na Liverpool kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wakati wa kupiga picha za kabla ya mcheo kuanza. Katika hali ya kawaida Ronaldo ni mmoja kati ya wachezaji wanaotambulika kuliko wachezaji wote duniani na amekuwa na tabia ya kujiongezea urefu ili azidi kuonekana mrefu kuwazidi wenzie na kuonekana kuliko wote. Hali hii imeonekana kwenye mchezo zaidi ya mmoja kiasi cha kuwa tabia ambayo inaendana na kile ambacho wengi wanaamini ni hulka binafsi ya Ronaldo ya kuwa na majivuno na mwenye kupenda kuonekana muda wote akiwa bora kuliko wenzie. Ronaldo hayuko peke yake katika hili kwani wiki chache zilizopita wachezaji wa Bayern Munich Dante na Jerome Boateng walionekana wakifunga jezi zao mgongoni ili waonekane 'wamejazia vifua' kuwatisha wapinzani .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako