• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nafasi ya kipa Meyiwa kwenye Klabu ya Olrando Pirates apewa Brighton Mhlongo

    (GMT+08:00) 2014-11-07 10:08:57

    Klabu ya Olrando Pirates ambayo bado iko kwenye lindi la majonzi ya kuondokewa na kipa wake namba moja na nahodha Senzo Meyiwa imemtangaza kipa Brighton Mhlongo kuwa ataanza kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Nedbank dhidi ya Supersports United utakaofanyika kesho jumamosi. Mhlongo ambaye alijiunga na Orlando Pirates tangu akiwa na umri wa miaka 14 amekuwa kipa wa akiba tangu wakati Senzo akiwa kipa namba mbili nyuma ya Moeneeb Josephs na sasa atapata nafasi ya kuonyesha ubora wake kufatia pengo lililoachwa na Senzo. Wachezaji wa Orlando Pirates wamekiri kuwa mchezo wao dhidi ya Supersport utakuwa mgumu kutokana na ukweli bado wako kwenye wakati mgumu baada ya kumpoteza mwenzao katika hali ya kutatanisha ambayo haikutarajiwa. Jukumu la Brighton Mhlongo litakuwa gumu hasa ukizingatia ukaribu aliokuwa nao yeye na marehemu Senzo enzi za uhai wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako