• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majina ya wachezaji bora wa Afrika wanaowania tuzo ya BBC kutajwa leo

    (GMT+08:00) 2014-11-10 11:55:57

    Asubuhi ya leo, BBC itataja majina matano ya wachezaji wa Afrika watakaoingia kwenye kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa mwaka wa Afrika. Huu ni mwaka wa 23, tangu tuzo hizo ziwatambue wachezaji bora wa Afrika wenye vipaji, baada ya mchezaji wa Ghana nahodha Abedi Pele kuchukua tuzo ya mwaka 1992 alipotambuliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika. Mbali na wachezaji hao nyota watano, kuna majina ya wachezaji wengi tu chipukizi ambao ndio bado wananoa vipaji vyao katika vilabu mbalimbali barani ulaya ambao nao wanapaswa kutambuliwa. Ushawishi wa wachezaji wa mwanzoni kama vile Ayew, George Weah na Nwankwo Kanu umepelekea hamu kubwa ya wachezaji wenye vipaji wa Afrika, na kupelekea kujulikana kwa wachezaji hao nyota wa kimataifa kwenye ligi kuu mbaliombali za Ulaya katika miaka ya 90.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako