Morocco imeshindwa kufikia tarehe ya mwisho kuthibitisha kama watakuwa wenyeji wa michuano ya Afcon Januari mwakani. Morocco ilishauri kuahirishwa kwa michuano hiyo kwa hofu ya mlipuko wa Ebola. Hata hivyo Caf ilikataa mara moja na kusisitiza kuwa shindano la wiki tatu litaendelea kama lilivyopangwa kuanzia Januari 17 hadi Februari 8 na badala yake kuipa hadi juzi Jumamosi tarehe 8 kutoa kauli yao ya mwisho kama wataandaa au la. Tarehe hiyo pia zilipewa nchi nyingine zote zinazotaka kujitolea na kuandaa michuano badala ya Morocco. Uamuzi wa mwisho utajulikana kesho Novemba 11 baada ya Caf kukutana kwenye kamati tendaji huko Cairo nchini Misri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |