• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsene Wenger akiri kuwa ubingwa ni ndoto msimu huu

    (GMT+08:00) 2014-11-12 10:22:30
    Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kwamba kichapo cha mabao 2-1 kutoka Swansea City kimemwondoa kwenye mbio za kusaka ubingwa msimu huu. Kocha huyo alikwenda ugenini kucheza mechi hiyo akiamini kwamba atapata pointi tatu na hivyo kuwa nyuma ya vinara Chelsea kwa pointi tisa lakini kwa sasa wapo nyuma ya kikosi cha Stamford Bridge kwa pointi 12. Licha ya kwamba walipata bao la kwanza kupitia Alexis Sanchez, Arsenal ilikubali kufungwa mabao mawili na wapinzani wao. Sasa Wenger amekiri kwa kusema Huwezi kukimbizana na timu ambayo imekupita kwa pointi 12, hiyo ni kazi ngumu sana. Wenger ambaye kikosi chake kwa sasa kipo nafasi ya sita nyuma ya Swansea City pia amekiri kwa makosa ya kuruhusu mabao, na anasema kosa kubwa ni kuruhusu umbali kutoka timu inayoshika nafasi ya kwanza na wao, wameachwa nyuma sana.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako