Zokora aitolea nje Ivory Coast baada ya kustaafu
(GMT+08:00) 2014-11-12 10:22:56
Didier Zokora amekataa nafasi ya kurejea tena kucheza kwenye timu ya taifa ya Ivory Coast kwa mechi mbili za mwisho za kufuzu kucheza kombe la matifa ya Afrika, baada ya kutangaza kustaafu. Kocha Herve Renard amemwita mchezaji huyo mwenye miaka 33 kwa ajili ya mechi dhidi ya Sierra Leone na Cameroon lakini alijibu kwa kusema uamuzi wa kustaafu mwezi Septemba bado anaushikilia na hautabadilika, kwani alichukua uamuzi huo mgumu baada ya kushauriana na shirikisho. Zokora ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Uturuki ni mchezaji aliyeichezea mara nyingi nchi yake zipatazo 121. Pia amecheza makombe matano mfululizo ya mataifa ya Afrika kati ya mwaka 2006 na 2013, lakini alisisitiza kuwa michuano iliyopita ni michuano yake ya mwisho. Hata hivyo kocha Renard alikuwa akitumai kuwa uzoefu wa Zokora ungesaidia kuboresha kikosi kwa vile tembo hao wanania ya kufufuzu fainali hizo. Hivi sasa wapo nafasi ya tatu kwenye kundi lao D ambapo tarehe 14 Novemba watacheza na Sierra Leone na siku 5 baadaye watakwaana na Cameroon.