Morocco kutoandaa fainali za Afcon, huku CAF ikitafuta nchi itakayookoa jahazi
(GMT+08:00) 2014-11-12 10:23:28
Nchi zote 28 zenye matumaini ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika zitaendelea na kampeni zake wikiendi hii, licha ya baada ya Shirikisho la soka la Afrika CAF kuthibitisha kuwa Morocco haitaandaa fainali hizo. Shirikisho hilo linaendelea kutafuta ni nchi gani itakayookoa jahazi la kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015. Morocco imeondolewa kutokana na kukataa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo mwakani kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola. Fainali hizo sasa huenda zikapelekwa Angola nchi iliyokuwa mwenyeji wa fainali hizo miaka minne iliyopita. Nchi nyingine zinazodhaniwa kuweza kuandaa mashandano hayo ni Gabon na Nigeria. Shirikisho la Soka la Afrika linasema litatoa uamuzi ni nchi ipi itakayoandaa mashindano hayo haraka iwezekanavyo.