• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bondia Emmanuel Shija wa Tanzania kukipiga na Mganda wikiendi hii

    (GMT+08:00) 2014-11-12 10:24:09
    Mtanzania anayefanya vizuri kwenye mchezo wa ndondi Emmanuel Shija hivi karibuni ataibeba bendera ya Tanzania nchini Uganda wakati atakapopanda ulingoni kupambana na Mganda Moses Golola katika pambano la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati. Pambano hilo linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii huko Jinja ambapo bondia toka Uganda Moses Golola amekuwa akijitamba kumpiga Mtanzania huyo ambaye kwa upande wake amekuwa mkimya akiamua kutojisifia sana na badala yake kufanya mazoezi ya nguvu ili aonyeshe uwezo wake siku ya pambano. Shija ana rekodi nzuri inayoonyesha kuwa katika mapambano 28 amefanikiwa kushinda mara 25 huku akipoteza mara tatu na hajatoka sare hata mara moja. Moses Golola amekuwa na kawaida ya kujisifu kwa mbwembwe nyingi kabla ya mapambano yake hali ambayo mwenyewe anadai inamsaidia kuwatia hofu wapinzani wake na kumpa faida ya kupata ushindi hata kabla ya kupanda ulingoni kwa kuwafanya wapinzani wake wapoteze hali ya kujiamini. Mara ya mwisho katika pambano lake Moses Golola alichakazwa na Mmarekani Richard Abraham katika pambano lililofanyika nchini Uganda.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako