Bingwa wa olimpiki wa mbio za mita 800 David Rudisha anatarajia kuwa ataendeleza ubabe wake safari hii kwenye mbio za mabingwa mwaka 2015 zitakazofanyika hapa Beijing China. Rudisha mwenye miaka 25, amesema kupata ushindi kwenye mbio hizi ndio lengo lake kuu, kwani msimu huu kwake yeye umekuwa mgumu sana. Akiwa bado anachangamoto kutoka kwa wakiambiaji wachanga Mohamed Aman, bingwa wa michezo ya ndani, Nijel Amos bingwa wa michezo ya nje na Timothy Kitum, mshindi wa medali ya shaba wa olimpiki, Rudisha amehakikishia watu kuwa atapambana na dhoruba hiyo.