• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Russia Igor Gamula apigwa marufuku kwa kauli za kibaguzi

    (GMT+08:00) 2014-11-13 15:44:19

    Shirikisho la Soka nchini Russia RES limetoa taarifa likisema kocha mkuu wa klabu ya FC Rostov Igor Gamula amesimamishwa kutoshiriki mechi tano baada ya kupatikana na hatia ya kutoa kauli za kibaguzi. Gamula ameadhibiwa kwa hivi karibuni kukiambia chombo cha habari kuwa klabu yake ina wachezaji wa kutosha wenye ngozi nyeusi, kwani wana sita kati ya vitu hivyo. Kocha huyo mwenye miaka 54 ameomba radhi kwa kila mchezaji nayehusika. Hata hivyo amesisitiza kuwa kauli yake hiyo alikusudia kufanya utani na kwamba ana uhusiano mzuri na wachezaji wote wenye ngozi nyeusi. Lakini waziri wa michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula na rais wa shirikisho la Soka la Afrika Kusini Danny Jordaan, wameitaka Fifa kulishughulikia suala hilo. Jordan amesema nchi yoyote ile itakayokuwa mwandaaji wa kombe la dunia inatakiwa kuwa mkarimu kwa taifa au rangi yoyote ile. Hivyo amesema anaamini kuwa Gamula anastahiki adhabu kali kwani hii sio mara ya kwanza kwa Russia kutoa matamshi kama hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako