Miaka takribani mitatu baada kuacha kuifundisha klabu ya FC Barcelona, kocha Pep Guardiola amezungumzia kama ikitokea nafasi ya kurudi Nou Camp hatakubali kuifundisha timu hiyo. Akizungumza na gazeti la Mundo Deportivo Guardiola ambaye alijiunga na Bayern Munich mwaka 2013 baada ya mapumziko ya mwaka mmoja tangu aondoke Barcelona amesisitiza kuwa haoni sababu ya kuweza kurudi kuifundisha klabu hiyo, kwa sababu alishamaliza kazi yake. Boss huyo wa Bayern Munich alitumia miaka minne Nou Camp akitengeneza timu hiyo ambayo inatajwa kuwa bora kuliko zote katika historia ya soka wakishinda makombe mawili ya ulaya na La Liga mara 3 kuanzia mwaka 2008 mpaka 2012. Baada ya miezi 12 ya mapumziko, Guardiola aliteuliwa kuwa kocha wa Bayern Munich mwaka jana, japokuwa mara kwa mara imekuwa ikiripotiwa kwamba anaweza kurejea kuifundisha Barcelona kwa muhula wa pili. Lakini wakati kocha huyo mwenye miaka 43 akiwa anakiri kwamba atarudi Catalonia kwenda kuishi na mkewe, anasema sio kwenda kuifundisha Barca tena.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |