• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ronaldo akanusha shutuma za kudhalilisha Messi

    (GMT+08:00) 2014-11-13 15:44:53

    Cristiano Ronaldo amekataa shutma kuwa amemsema vibaya kinara mwenzie katika soka, Lionel Messi. kitabu kipya kuhusu mshambuliaji huyo wa Barcelona, kinaeleza kuwa mchezaji wa Real Madrid mara kwa mara amekuwa akitumia maneno ya kudhalilisha dhidi ya Messi. Kumekuwa na tetesi kwa muda mrefu juu ya kutoelewana kwa Ronaldo na Messi. Ronaldo amesema kuwa hizi ni habari za uongo na kusema kuwa atachukua hatua za kisheria kuwashtaki wanaohusika na usambazaji wa taarifa hizo. Mchezaji huyo amejitetea kuwa anawaheshimu wachezaji wenzake wote, akiwemo Messi. Ronaldo amemaliza ubabe wa Messi wa kutwaa tuzo ya Fifa ya mchezaji bora wa dunia kwa miaka mitatu mfululizo, Ballon d'Or baada ya kutwaa tuzo hiyo mwaka jana. Zaidi ya yote nyota hao wametofautiana kwa goli moja tu ili kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya. Messi ana magoli 71 sawasawa na Raul Gonzales wakati Ronaldo ana magoli 70. Messi anahitaji magoli mawili tu ili kuwa mfungaji bora wa muda wote wa ligi kuu ya Hispania La Liga, amefunga magoli 250 katika michezo 285 nyuma ya Telmo Zarra wa Athletic Bilbao aliyecheza miaka ya 1940-1950.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako