Qatar inatarajiwa kusafishwa na shutuma za ufisadi wakati wa kinyang'anyiro cha kuwania kuwa nchi mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022. Ilidaiwa kuwa Qatar ilishinda baada ya maafisa kupewa rushwa ya pauni milioni 3 ili kuipigia kura nchi hiyo. Qatar ilikabidhiwa kuandaa michuano hiyo mwaka 2010 na kuzishinda nchi kama vile Australia, Marekani, Korea Kusini na Japan. Uamuzi huo uliwashangaza wengi na hatimaye kupelekea tuhuma nyingi za rushwa. Wakili wa Marekani Michael Garcia alipewa kazi ya kuchunguza madai hayo na baada ya kuwahoji watu wanane wanaohusishwa na tuhuma hizo amewasilisha ripoti mapema mwezi wa Septemba. Baada ya kuangaliwa kwa kina ripoti hiyo na jaji wa Ujerumani alifupisha ripoti ambayo inatarajiwa kutangazwa leo. Ripoti hiyo sio tu imesaifisha Qatar bali pia inaaminika kuwa imelionya shirikisho la soka la Uingereza kwa tabia yake wakati wa mchakato wa kinyang'anyiro hicho.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |