• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais Xi Jinping nchini Australia kuimarisha uhusiano kati ya China na Australia

    (GMT+08:00) 2014-11-13 19:58:33

    Naibu waziri wa mambo ya nje ya China Zheng Zeguang amesema, ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini Australia itakuwa na umuhimu mkubwa katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Wakati wa ziara hiyo itakayofanyika kati ya tareha 16 hadi 23, rais Xi pia atahudhuria mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 utakaofanyika mjini Brisbane.

    Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya rais wa China nchini Australia katika miaka 7 iliyopita.

    China ni mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Autralia, na thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili imefikia dola za kimarekani bilioni 130. China pia ni chanzo kikubwa zaidi cha wanafunzi na watalii nchini Autralia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako