• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka nchi za BRICS kushiriki kikamilifu katika uongozi wa uchumi duniani

    (GMT+08:00) 2014-11-15 20:01:41

    Rais Xi Jinping wa China amesema nchi za kundi la BRICS zinatakiwa kushiriki kikamilifu katika ushirikiano wa kimataifa na kufanya sauti zao zisikike katika uongozi wa uchumi duniani.

    Akizungumza kwenye mkutano na viongozi wa nchi za BRICS mjini Brisbane, rais Xi amesema ushirikiano wa kiuchumi ndio nguvu pekee kwa maendeleo ya nchi za BRICS. Amesema nchi za BRICS yaani Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zinatakiwa kujitolea katika kuunda mwongozo wa muda mrefu wa ushirikiano wa kiuchumi kwa kuunganisha masoko, kuhimiza mafungamano ya kifedha, kuunganisha miundo mbinu pamoja na mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo.

    Aidha viongozi wa nchi za BRICS wameelezea wasiwasi wao juu ya kutotekelezwa kwa mageuzi ya mwaka wa 2010 katika Shirika la Kimataifa la Fedha IMF. Kwenye taarifa yao, viongozi hao wamekubaliana kuwa ucheleweshwaji wa mageuzi ya IMF kunahujumu uhalali na uaminifu wa shirika hilo la IMF.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako