• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ashiriki kwenye mkutano wa 9 wa viongozi wa kundi la G20

    (GMT+08:00) 2014-11-15 20:32:09

    Mkutano wa 9 wa viongozi wa kundi la G20 umefunguliwa rasmi mjini Brisbane, Australia. Rais Xi Jinping wa China amehudhuria mkutano huo na kutoa hotuba.

    Ajenda kuu ya mkutano huo ni kuhimiza ongezeko la uchumi na ajira, pamoja na kuongeza uwezo wa uchumi wa dunia katika kukabiliana na hatari zinazoweza kutokea. Makubaliano yanayotarajiwa kufikiwa kwenye mkutano huo yanajumuisha mambo ya nishati, maendeleo, biashara, ajira, vita dhidi ya ufisadi, mambo ya kifedha, uwekezaji wa miundo mbinu, mageuzi katika mashirika ya fedha ya kimataifa, usimamizi wa fedha na kodi.

    Kwa mujibu wa mwaliko wa waziri mkuu wa Australia, rais Xi Jinping wa China jana aliwasili Brisbane kushiriki kwenye mkutano huo wa kundi la G20 na kufanya ziara rasmi nchini Australia.

    Rais Xi amesisitza kuwa, anatarajia kushirikiana na viongozi wengine wa nchi wanachama wa kundi la G20 kusukuma mbele kazi ya kushughulikia uchumi wa dunia, kukabiliana na changamoto kwa pamoja ili kuleta maendeleo na ustawi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako