• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuhimiza ukuaji na kutoa mchango kwa uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2014-11-16 20:02:12
    Rais Xi Jinping wa China amesema China itaendeleza kasi ya ukuaji wa uchumi na kutoa mchango mkubwa kwa uchumi wa dunia.

    Akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa kundi la G20 nchini Australia, rais Xi ameyataka makundi ya kiuchumi duniani kufanya mageuzi kwa pamoja, kutekeleza kikamilifu mikakati ya ukuaji na kuharikisha mchakato wa kufufua uchumi wa dunia na kupata ongezeko endelevu.

    Xi amesema kitu kinachotakiwa kupewa kipaumbele hivi sasa na kundi la G20 ni kuratibu sera za uchumi jumla kukabiliana na athari za kiuchumi, kuunda nafasi za ajira na kuimarisha maisha ya watu.

    Rais Xi amesisitiza kuwa mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki APEC uliomalizika hivi majuzi mjini Beijing ulifanikiwa kuunda mwongozo wa kuhimiza maendeleo katika eneo la Asia na Pasifiki na kuongeza kuwa nchi za kundi la G20 pia zimeunda mikakati dhabiti ya ukuaji.

    Viongozi wengine wa G20 wamepongeza juhudi za China za kufanyia mageuzi uchumi wake na kusisitiza kuwa wana matumaini kuwa uchumi wa China utaendelea kukua na kutoa mchango mkubwa kwa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako