Cristiano Ronaldo kusaini mkataba mpya na Real Madrid
(GMT+08:00) 2014-11-18 09:43:21
Cristiano Ronaldo amesema anataka kuendelea na mkataba wake na Real Madrid, ambapo bado ana miaka karibu minne ya kuendelea na kalabu hiyo. Mholanzi huyo mwenye miaka 29, amekuwa akihusishwa kurejea Manchester United, ambayo aliondoka kujiunga na Real mwaka 2009 kwa ada ya pauni milioni 80. Ronaldo amepewa kiatu cha dhahabu kwa kuwa mfungaji bora wa Ulaya ambapo aliingiza magoli 31 katika ligi ya La Liga mwaka 2013-14. Ronaldo amesisitiza kuwa anatarajia kumaliza mkataba wake na Real akiwa na miaka 33 na baada ya hapo ataangalia kama bado watataka aendelee kuwepo Real au la. Ronaldo amepata pamoja kiatu hicho cha dhahabu na mchezaji wa Uruguay Luis Suarez ambaye naye pia ana magoli 31 katika ligi ya England kwa msimu ulioipita akiwa na Liverpool kabla ya kujiunga na Barcelona kwa ada ya pauni milioni 75. Akizungumza kupitia tovuti ya Real Ronaldo amesema atafanya majadiliano na rais wa klabu hiyo Florentino Perez juu ya kuendeleza mkataba wake ambao alisaini Septemba mwaka jana.