• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michael Platini ataka mashindano ya kombe la dunia ya Qatar yafanyike majira ya baridi

    (GMT+08:00) 2014-11-18 09:43:43
    Rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya Michael Platini amesema mashindano ya kombe la dunia ya Qatar mwaka 2022 ni lazima yafanyike katika msimu wa baridi. Msimamo wake huo umemuweka kwenye upinzani wa moja kwa moja na baadhi ya ligi kubwa za ulaya pamoja na klabu ambazo zinataka michuano ifanyike mwezi Mei. Kombe la dunia kawaida linafanyika mwezi Juni na Julai. Lakini Fifa imeambiwa kuwa joto la Qatar katika majira ya joto litahatarisha afya za wachezaji. Platini alisema haitakuwa mwezi Aprili, Mei au Juni, bali iwe katika majira ya baridi, na kuongeza kuwa nusu fainali na fainali za ligi ya mabingwa wa Ulaya zinaweza kuhamishiwa mwezi Juni kama kuna ulazima akisisitiza kuwa klabu zitakubali uamuzi wowote utakaofikiwa. Ligi ya England, ligi ya Hispania La Liga na Bundesliga ya Ujerumani zinaona kuwa mashindano ya kombe la dunia yakifanyika Mei hayatasababisha usumbufu mkubwa, ambapo Fifa inatafuta tarehe mbadala ya Juni na Julai.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako