• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji wa Tanzania Mrisho Ngassa amaliza akiwa kinara wa kufunga mabao mengi Ligi ya Mabingwa Afrika

    (GMT+08:00) 2014-11-18 09:44:29
    Mshambuliaji wa klabu ya Yanga ya Tanzania, Mrisho Ngassa amepata zari Afrika, baada ya kumaliza akiwa kinara wa kufunga mabao mengi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, licha ya klabu yake kuaga mashindano hayo alfajiri kabisa. Ngassa amemaliza akiwa kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria. Ni baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufikia tamati wikiendi iliyopita na ES Setif kutangazwa mabingwa wapya. Ngassa aliyafunga mabao hayo katika raundi ya kwanza walipocheza na Komorozine ya Comoro mchezo wa kwanza walishinda 7-0 na marudiano walitoka kifua mbele kwa mabao 5-2. Yanga ilitolewa kwenye mashindano na Al Ahly ya Misri kwa penalti 3-4. Lakini Ngassa hawezi kupewa zawadi yoyote kwavile wamefungana na kiutaratibu hata mchezaji akishinda tuzo hiyo CAF huitoa kwa klabu yake.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako