CAF ina wasiwasi kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola
(GMT+08:00) 2014-11-18 09:45:13
Shirikisho la soka barani Afrika CAF lina wasiwasi kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, licha ya kukataa ombi la kuahirisha michuano hiyo ya mwaka 2015 barani Afrika. Waandaaji wa michuano hiyo Morrocco wana hadi kesho Jumamosi kuamua iwapo bado wanataka kuandaa mechi hizo. Wana hofu ya kuandaa michezo hiyo kutokana na mlipuko wa Ebola magharibi mwa Afrika. Katibu mkuu wa Caf Hicham El Amrani amesema wana wasiwasi kuhusu hali yote kwani si hali nzuri kwa wao wote. Lakini alisisitiza kuwa wanaelewa tahadhari ambayo taifa huru lina haki kuchukua, ila ni muhimu kutoongeza hofu na badala yake kuwa wazi kuhusu vile unavyoweza kuambukizwa kutoka eneo moja hadi jingine huku ikichukuliwa tahadhari. Katibu huyo ameongeza kuwa wamekuwa wakifanya kazi na Shirika la Afya Duniani tangu mwezi aprili ili kuhakikisha kuwa hakuna hatari zozote. Na Hawawezi kujiweka katika hatari yoyote iwapo hawajui kwamba mashindano hayo ni tishio kwa mwandaaji.