• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachangia ujenzi wa maabara ya kuzuia magonjwa nchini Sierra Leone

    (GMT+08:00) 2014-11-21 11:03:43

    Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone jana alikabidhi eneo la ujenzi wa maabara ya kudumu inayofadhiliwa na China ambayo inalenga kufanya majaribio ya bakteria na magonjwa mengine nchini humo.

    Akiongea kabla ya kukabidhi eneo hilo, rais Koroma alisema anatarajia kuwa kituo cha kuzuia magonjwa CDC, sio tu kitahudumia Siera Leone bali kanda nzima. Amesisitiza kuwa China sio tu ina nia ya kutoa wafanyakazi wa afya kwenye maabara hiyo, lakini pia imeahidi kuwafunza wafanyakazi wa nchi hiyo ili waweze kutoa huduma wao wenyewe hapo baadaye. Kwa upande wake balozi wa China nchini Sierra Leone Zhao Yanbo amesema China sio tu itashughulikia msukosuko wa Ebola uliopo sasa, bali pia itasaidia kwenye msukosuko huo kwa njia ya kubadilisha mfumo wa afya nchini humo.

    Wakati huohuo serikali ya China jana ilichangia vifaa vya matibabu vyenye thamani ya dola laki 8.2 za kimarekani ili kusaidia Togo kuzuia ugonjwa wa Ebola. Vifaa hivyo ni pamoja na nguo, miwani ya kujikinga na vifaa vingine vya matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako