Bodi ya utalii nchini Uganda UTB imesema kuwa sasa itatumia kampuni ya uhusiano mwema ili kuuza Uganda kitalii katika mataifa ya nje.
Bodi hiyo inasema itafanya hivyo baada ya harakati za kuimarisha utalii nchi humo mwaka huu kuandikisha matokeo duni.
Naibu afisa mkuu wa bodi hiyo John Ssempebwa anasema mpango huo tayrai umeanza katika mataifa ya Marekani na Ulaya na hivi karibuni itaanza Asia.
Hata hivyo afisa huyo hajataja ni Kampuni gani imepewa kufanya kazi hiyo.
Uganda kama majirani zake kama vile Kenya Rwanda na Tanzania utegemea sana utalii katika kuleta mapato ya kigeni.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |