• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Spika wa Bunge la Umma la China aanza ziara nchini Peru

    (GMT+08:00) 2014-11-21 19:47:46

    Spika wa Bunge la Umma la China ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China Zhang Dejiang amewasili mjini Lima, Peru jana, na kuanza ziara nchini humo inayolenga kuinua uhusiano kati ya mabunge ya China na Peru na pia kati ya nchi hizo mbili.

    Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na spika wa Bunge la Umma la China tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi mwaka 1971. Akiwa nchini Peru, Zhang atakutana na rais wa nchi hiyo Ollanta Humala Tasso, na pia kufanya mazungumzo na spika wa bunge la Peru, Ana Maria Solorzano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako