• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chelsea na Manchester City zaendeleza kungarisha nyota zao ligi kuu England

    (GMT+08:00) 2014-11-24 15:06:26
    Chelsea imeendelea kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 32 bila mpinzani baada ya kuilaza West Brom kwa mabao 2-0. Nao, Manchester City waliilaza Swansea kwa mabao 2-1 katika mchezo mwingine wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Etihad. Mabao ya Diego Costa na Eden Hazard, kipindi cha kwanza yaliiwezesha Chelsea kuibuka na ushindi dhidi ya West Brom iliyocheza muda mrefu na wachezaji 10 baada ya Claudio Yacob kutolewa kwa kadi nyekundu. Swansea walitangulia kufunga bao kupitia kwa Wilfried Bony kabla ya Steven Jovtric kusawazisha na Yaya Toure kumaliza kazi, kipindi cha pili. Waka ti huohuo Hali kwenye klabu ya Liverpool imeendelea kuwa mbaya baada ya kupoteza mchezo wake wa tatu mfululizo kwenye ligi hiyo. Liverpool iliuona uwanja wa Selhurst Park mchungu baada ya kufungwa 3-1 kwenye mchezo wao dhidi ya Crystal Palace. Wekundu hao wa huko Anfield walianza kufunga kupitia Ricky Lambert ambaye alikuwa anafunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Liverpool akitokea Southampton. Hata hivyo Crystal Palace ilirudisha mabao hayo kupitia kwa Mile Jedinak, Dwight Gayle na Joe Ledley. Matokeo haya yanaifanya Liverpool ibaki kwenye nafasi ya 12 baada ya kupoteza michezo 6 kati ya 12 ya msimu huu kwenye ligi ya England. Kwingineko matokeo yalikuwa Everton 2-1 West Ham, Newcastle 1-0 QPR, Stoke 1-2 Burnley, Leicester 0-0 Sunderland.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako