Mshambuliaji wa klabu ya Yanga ya Tanzania, Genilson Santos 'Jaja' ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo na nafasi yake itazibwa na kiungo mkabaji pia raia wa Brazil, Emerson Oliveira Neves Roque. Jaja, ambaye yuko nchini kwao Brazil kwa mapumziko mafupi ya Ligi Kuu hatarejea Tanzania na sasa kocha mkuu wa Yanga, Marcio Maximo atarejea kesho Jumanne jijini Dar es Salaam akiwa na Emerson pamoja na kiungo mwingine wa timu hiyo, Andrey Coutinho. Ingawa inaelezwa kuwa Jaja hatarudi kutokana na matatizo ya kifamilia, lakini presha kubwa aliyokuwa akiipata kwa mashabiki imechangia hilo na hivyo Maximo kuona ni bora ampumzishe kwani akiendelea kumng'ang'ania hata yeye anaweza kutimuliwa.