• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakamilisha ujenzi wa kituo cha matibabu ya Ebola nchini Liberia

    (GMT+08:00) 2014-11-26 10:31:00

    Ujenzi wa kituo chenye vitanda 100 cha kutibu wagonjwa wa Ebola huko Monrovia, kilichojengwa kwa msaada wa serikali ya China umekamilika. Naibu mkurugenzi wa kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China Bibi Cui Li amesema kwenye shughuli ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kuwa, vikundi vitatu vya madaktari 500 wa China watafanya kazi katika kituo hicho, na kutoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi wa Liberia. Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia ameishukuru China kwa msaada inaotoa kwa Liberia katika kupambana na Ebola.

    Na Shirika la Afya Duniani WHO limeonya kuhusu kutokuwepo kwa malengo ya kuchukua hatua katika baadhi ya sehemu ya Afrika ya magharibi, wakati watu wengine wawili nchini Mali wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola.

    Sierra Leone, Liberia na Guinea zimeathiriwa zaidi Ebola, Senegal na Nigeria ambazo pia ziliathiriwa na ugonjwa huo sasa hakuna Ebola. Mali, ambayo haikuwa na virusi vya Ebola, sasa inapambana na ugonjwa huo.

    Habari nyingine zimesema Ethiopia imetangaza kuwa itatuma watu 210 wanaojitolea ndani ya wiki mbili kwenda nchi zilizokumbwa na Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako