• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yasherehekea mkataba wa dunia juu ya haki za watoto

    (GMT+08:00) 2014-11-26 11:09:28

    Uganda imeadhimisha miaka 25 ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa haki za watoto, kwa kueleza nia ya kuzidi kuheshimu haki za watoto.

    Katika kongamano lililofanyika huko Kampala chini ya kauli mbiu ya "kutegemea kuongeza haki za watoto", mke wa rais wa Uganda bibi Janet Museveni amesema licha ya maendeleo makubwa yaliyofikiwa bado kuna pengo ambalo linahitaji kujazwa. Amesema wakati taifa likiwa na wajibu wa kuwatunza watoto, wazazi lazima watimize majukumu yao. Amefafanua kuwa kazi inayofanywa na familia haiwezi kudharauliwa, kwani familia ina kazi ya kuwalinda, kuhakikisha afya na kuwapatia elimu watoto.

    Naye mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF nchini Uganda Bibi Aida Girma amesema, Uganda ni kiongozi duniani katika kuendelea kutafuta njia za kumfikia kila mtoto, hasa wale walioachiwa nyuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako