• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajeshi wa Yemen wawakomboa mateka 6 waliokuwa wakishikiliwa na al-Qaida

    (GMT+08:00) 2014-11-28 10:50:48

    Wizara ya ulinzi ya Yemen imesema wanajeshi wa kupambana na ugaidi nchini humo wamewaokoa mateka sita kutoka kwa kundi la al-Qaida wiki hii, lakini bado wanaendelea kuwatafuta wengine watano, wakiwemo raia wa Marekani, Uingereza na Afrika Kusini.

    Ikimnukuu ofisa mmoja aliyeshiriki kwenye operesheni ya uokoaji, wizara hiyo imesema wanajeshi hao waliongoza operesheni ya kuwakomboa mateka sita, wakiwemo raia wa Saudi Arabia na Ethiopia na kuwaua watekaji nyara saba wa al-Qaida. Hata hivyo amesema bahati mbaya wameshindwa kuwakomboa wengine watano kwasababu walihamishiwa sehemu nyingine siku mbili kabla ya operesheni kuanza.

    Maofisa wa Yemen wamesema wanajeshi wa Marekani pia walishiriki kwenye operesheni hiyo iliofanyika Jumatatu usiku katika mkoa wa Hadramout ambako kuna wafuasi wengi wa kundi la al-Qaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako