• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yatenga Dola Bilioni 20 kutumika kuendeleza uzalishaji wa kawi.

    (GMT+08:00) 2014-11-28 19:36:23

    Katika awamu ya pili ya uendelezaji wa uzalishaji wa kawi nchini Ethiopia nchi hiyo imetenga Birr Bilioni 20, kutumika kuendeleza uzalishaji wa kawi nchini humo katika kipindi kati ya mwaka wa 2015 na 2020.

    Afisa mkuu wa mipango katika idara ya uendelezaji wa kawi nchini humo Mukuria Lemma, amesema mpango huo unakubalika na serikali ya nchi hiyo na huko katika mipango yake ya kufikia uzalishaji wa kawi ya kutosha nchini humo, pamoja na mauzo ya nje ya nchi.

    Kwa mujibu wa idara hiyo ni kwamba fedha hizo zitatumika kujenga miradi 10 hadi 12, ya kuzalisha umeme na pia kuimarisha ya sasa katika juhudi, za kufikia lengo la kuzalisha megawati 6,000 za umeme kote nchini Ethiopia.

    Serikali ya Ethiopia pia imetangaza kuwa itapunguza kwa asilimia kubwa kodi ambazo, hutozwa wawekezaji wa kigeni nchini humo pindi tu uzalishaji wa umeme nchini, utakapofikia fikia viwango vya vinavyohitaji kupunua kwa ada za umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako