• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uliokuwa mradi wa kwanza wa kawi nchini Ethiopia kuanza kuzalisha umeme tena

    (GMT+08:00) 2014-11-28 19:36:51

    Uliokuwa mradi wa kwanza kuanza kuzalisha umeme nchini Ethiopia utaanza kazi tena, baada ya kusimamisha kazi zaidi ya miaka 40 iliyopita.

    Mradi huo kwa jina Aba Samuel utaanza kufanya kazi tena katika muda wa miaka miwili ijayo, baada ya kufanyiwa ukarabati kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

    Ukarabati huo umekuwa ukifanywa na Kampuni ya Hydrochina Houdong, kwa gharama ya Dola milioni 20 ambazo milioni 15 zilitolewa na serikali ya Marekani na milioni 5 na serikali ya Ethiopia.

    Afisa mkuu mtendaji wa shirika la kawi nchini humo EEP Bi.Azeb Asnake, anasema ni kwamba pia mradi huo ukikamilika utatumika kama eneo la kitalii nchini humo.

    Mradi huo ulio katika mto Akaki ulianzisha mwaka wa 1936, na ukaacha kufanya kazi katika mwaka wa 1974, baada ya mashine zake kuharibika, ambapo ilikuwa ikizalisha megawati 6, lakini haijaarifiwa itakuwa itakuwa ukizalisha megawati ngapi baada ta kuanza kazi upya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako