• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuandaa wafanyakazi 4,000 wa kupambana na Ebola kwa ajili ya Sierra Leone

    (GMT+08:00) 2014-12-04 10:08:33

    Wafanyakazi 600 wa matibabu wa Sierra Leone wamemaliza mafunzo ya wiki tatu yaliyoandaliwa na wataalam wa matibabu wa China wanaosaidia nchi hiyo kupambana na Ebola.

    Mkuu wa programu ya mafunzo ya afya ya umma ya China nchini Sierra Leone Liang Xiaofeng amesema,

    "Programu hiyo inatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa serikali, maofisa wa polisi, vikosi na wafanyakazi wa matibabu. Tunapanga kutoa mafunzo kwa watu 10,000 barani Afrika, wakiwemo 4,000 kutoka Sierra Leone. Nina matumaini kuwa kuwasili kwetu kumeongeza imani ya watu wa Afrika, hasa wa Sierra Leone katika mapambano dhidi ya Ebola."

    Mlipuko wa Ebola barani Afrika mwaka huu umesababisha vifo vya watu elfu 7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako