• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utamaduni wa kunywa kahawa nchini China

    (GMT+08:00) 2014-12-04 14:58:49

    Leo kwenye kipindi hiki tunazungumzia utamaduni mpya unaojitokeza katika jamii ya China, yaani utamaduni wa kunywa kahawa, na jinsi unavyopokelewa na wenyeji.

    Pili: Katika hali ya kawaida wachina ni watu wanaopenda kunywa chai. Kahawa naweza kusema ni utamaduni wa kigeni kabisa kwao, lakini kwa sasa ukiwa hapa China na hasa kwenye miji mikubwa, karibu kila mahali kuna migahawa ya chai. Karibu migahawa yote ni ya kimagharibi kama vile Starbucks, Costa coffee na mingine. Kwa hiyo kwa upande fulani tunapozungumzia unywaji kahawa hapa China hatuzungumzii utamaduni wa jadi wa China, tunazungumzia utamaduni ambao ndio unaanza kuenea.

    Fadhili: Kwa wasikilizaji wetu ambao wamebahatika kutazama filamu za kichina, hasa filamu kama za Jackie Chan na Bruce Lee watakuwa wanakumbuka kuwa mara kadhaa Jackie Chan anaonekana akinywa chai na mwalimu wake, au watu wanakuwa mitaani wakiwa kwenye migahawa ya chai, lakini sio migahawa ya kahawa.

    Pili: Lakini nadhani kwenye hizi video ambazo huwa tunaangalia kuhusu China, labda hazielezi kwa undani maana hali ya Chai. Wanaotazama kwenye video wanaweza kudhani wachina wanakunywa chai kama tu wana kiu ya chai, au kupata ladha ya chai. Lakini ukweli kuhusu chai ni zaidi ya hapo. Wachina wanakunywa chai karibu kila mahali walipo, nyumbani, kazini au hata safarini, na uandaaji wao wa chai una umaalum wake, wakati mwingine hata unywaji una umaalum wake.

    Fadhili: Lakini kuna wakati wanaweza kuandaa chai kwa njia rahisi kabisa. Wanahitaji maji ya moto na majani ya chai, wanaweka majani kwenye maji halafu wanakunywa, hakuna haja ya kutia sukari au hata maziwa. Sisi kule nyumbani kuandaa chai ni mchakato mrefu kiasi, lakini vilevile hata utamaduni wa kunywa chai haufanani na wa hapa.

    Fadhili: Ni vizuri tukisikiliza maoni ya wasikilizaji wetu kuhusu unywaji wa kahawa. Tuanze na maoni ya vijana wa hapa China tusikie wanasemaje kuhusu kahawa Tuanze na Bibi Wang Mengdie

    Naona sababu kuwa ni kwamba hivi sasa watu wanapenda vitu vya haraka, kwa mfano Fastfood. Lakini unywaji wa chai unachukua muda mwingi. Kunywa kahawa ni tofauti, wachina wengi hawafahamu undani wa kahawa, wanaona kunywa kahawa ni mtindo mpya wa maisha tu, kwa hivyo vijana wengi wanapenda sana kahawa, na wanaichukulia kama ni utamaduni wa maisha ya haraka.

    Fadhili: Bi Wang anaona utamaduni wa sasa wa watu kunywa kahawa unafuata mtindo wa maisha, watu wanaenda mbiombio, kwa hiyo hawana muda wa kukaa kuandaa chai, na kuanza kunywa, badala yake wanaona wakinunua kahawa ni rahisi, tena wanaweza kubeba na kuondoka nayo.

    Pili: Hiyo nadhani ni tofauti moja iliyopo kati ya Chai na kahawa, chai mara nyingi inahitaji ukae utulie upike na unywe, si kitu cha haraka. Labda tumsikilize Bw Wang Yu naye ana maoni yanayofanana na ya bi Wang kuhusu kahawa

    Naona ni jambo la kwenda na wakati, yaani utamaduni wa nchi za magharibi na vitu vya kisasa vimeingia kwenye maisha ya wachina. Kwa hiyo watu, hasa vijana, wanafahamu mtindo wa maisha ya kimagharibi kupitia filamu, vitabu na njia nyingine, na pia wanapenda kuonyesha umaalum huo kwenye maisha yao mwenyewe. Wanaona kukutana na marafiki kwenye mgahawa wa kahawa ni mtindo mpya wa maisha. Kwa upande mwingine, sidhani kahawa itachukua nafasi ya chai. Kwa sababu wachina tumekuwa tunatumia chai kwa karne nyingi, na imekuwa ni desturi ya wachina. Ingawa leo ninakunywa kahawa, lakini napenda chai zaidi. Naona chai inafaa zaidi kwa wachina, na inafaa zaidi kiafya.

    Pili: Hapa kwenye utamaduni ndio kuna tofauti kiasi. Wenzetu huwa wanakwenda kwenye migahawa ya chai kama wanataka kuongea kuhusu jambo fulani, migahawa inakuwa ni sehemu ya mazungumzo huku wanakunywa chai. Inawezekana wanachagua chai yenye ladha fulani lakini chai yenyewe sio jambo hasa linalowapeleka kwenye mgahawa wa chai.

    Fadhili: Lakini sasa tunaanza kuona kuwa Kahawa inachukua nafasi ya Chai, au tunaweza kusema inakuwa na nafasi kama Chai. Ila kuna tofauti kuhusu migahawa yenyewe ya chai, kwa mfano hii migahawa ya Starbucks, Costa Coffee, na mingine ni ya kimagharibi sana. Karibu kila kitu kimekaa kimagharibi, kwanza majengo yake, viti vyake na hata ladha ya kahawa yenyewe na vinavyochanganywa kwenye kahawa.

    Pili: Lakini la muhimu zaidi ni kuwa wachina wanapokutana kwenye maongezi fulani huwa wanakunywa chai. Chai huwa inasindikiza tu mazungumzo, yenyewe sio lengo kuu. Kwenye mazingira mengine ambayo naweza kusema ni mazuri kidogo kuliko nyumbani, chai huwa hailevyi, kwa hiyo kama mnaongea na kunywa chai, hammalizi maongezi kwa kulewa, kama wanaofanya hivyo huku wakinywa bia.

    Fadhili: Nimewauliza baadhi ya wasikilizaji wetu kuhusu utamaduni wa kunywa chai au kahawa kule nyumbani Afrika Mashariki, lakini wengine wanasema kwenye nchi zetu tatizo sio Chai na Kahawa, ni Chai na Pombe au Chai na Kahawa, na moja ya hivyo viwili vinatumika kwenye maongezi, na kuwa na matokeo tofauti.

    Pili: Naona hapa kuna suala la utamaduni na aina ya mikusanyiko, lakini Bwana Ombati anaona Chai katika hali ya kawaida inafaa zaidi. Maoni yake pia yanafanana na Bi Zena kutoka Bujumbura ambaye

    Fadhili: NI kweli Chai bila shaka haina usumbufu wala matatizo kwa mnywaji, najua kuwa kwenye nchi zetu chai inanywewa zaidi kuliko kahawa, na hata kuliko bia.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako