Sehemu ya Pili: Maua mia yachanua
--Kupatana na kuingiliana kwa tamaduni za aina mbalimbali
Njia ya Hariri kwenye bahari iliyosifiwa pia kuwa ni "Njia ya biashara ya vyombo vya kauri baharini", na "Njia ya biashara ya viungo vyenye harufu nzuri baharini", ilikuwa njia kubwa ya biashara ya kimataifa katika zama za kale. Kuanzia Enzi za Qin na Han (mwaka 221 kabla ya Kristo--mwaka 220), wachina walisafirisha Hariri na bidhaa nyingine hadi India kupitia njia hiyo. Katika zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, si kama tu bidhaa za viungo vinavyonukia vizuri, pembe za ndovu na vito zilizozalishwa sehemu mbalimbali duniani zilisafirishwa hadi nchini China kupitia njia hiyo baharini, bali pia bidhaa za Hariri, Vyombo vya Kauri na Chai za China zilisafirishwa na kuuzwa India na Afrika.
(1) Njia ya Biashara ya Vyombo vya Kauri
Katika karne ya 13, shughuli za utengenezaji wa vyombo vya kauri zilididimia siku hadi siku katika sehemu ya mashariki ya kati, hivyo wafanyabiashara waliojishughulisha na biashara kwenye njia ya baharini walianza kufuatilia vyombo vya kauri vya China. Ingawa kulikuwa na vyombo vya kauri vya rangi ya kijani vya Enzi ya Song ya China(mwaka 960--1279)vilivyofukuliwa katika sehemu mbalimbali barani Afrika, lakini ilipofika katikati ya Karne ya 14, ndipo vyombo vya kauri vya China vilipoanza kusafirishwa hadi pwani ya Afrika mashariki.
Hivi leo katika Jumba la makumbusho la taifa la Tanzania kuna vyombo vya kauri vya China vipatavyo zaidi ya mia moja vilivyofukuliwa huko, mbali na mabaki machache ya Enzi ya Yuan(mwaka1271--1368), vingi ni vyombo vya kauri vyenye thamani vya Enzi za Ming na Qing za China(mwaka1368--1912) vilivyosafirishwa na kuuzwa ng'ambo, vyombo hivyo vinaweza kuthibitishana na vile vilivyofukuliwa kwa wakati mmoja nchini China.
|