Kilabu ya Manchester United iliendelea kuonyesha makali yake baada ya kuiadhibu vikali Liverpool mabao 3-0 katika mechi ya kasi iliojaa mashambulizi makali kutoka pande zote mbili.
Hatahivyo dakika chache baadaye, Manchester U waliona lango la Liverpool kupitia nahodha wao Wayne Rooney katika kipindi cha kwanza. Yuan Mata alifanya mambo kuwa mbili bila baada ya kufunga krosi safi kutoka kwa Ashley Young, bao ambalo wachezaji wa Liverpool walidhani ni la kuotea. Licha ya Liverpool kunoa safu yao ya mashambulizi na kuvamia ngome ya Manchester United kupitia Sterling aliyekosa mabao ya wazi Manchester united iliendelea kufanya mashambulizi kupitia Van Persie na Rooney. Liverpool ilimuingiza Mario Balotelli ambaye pia naye alikosa mabao ya wazi. Baada ya dakika kadhaa, Robin Van Persie alifanya mambo kuwa 3-0 baada ya safu ya ulinzi ya Liverpool kufanya masihara katika lango lao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |