• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Khan atetea taji lake kwa kushinda kumbwaga Devon Alexander wa Marekani

    (GMT+08:00) 2014-12-15 15:53:23

    Bondia wa Uingereza Amir Khan ametetea taji lake la uzani wa Welterweight kwa wingi wa pointi dhidi ya bondia wa Marekani Devon Alexander mjini Las Vegas. Baada ya Khan mwenye umri wa miaka 28 kutawala raundi za mapema, Alexander alitoa upinzani hafifu hadi raundi ya 8 alipoanza kumpa Khan makonde mazito. Lakini Khan ambaye anasifika kwa wepesi wake wa kurusha makonde aliendelea kudhibiti pigano hilo huku majaji wote wakimpatia ushindi. Baadaye Khan alisisitiza mpango wake wa kutaka kuzichapa na bingwa wa dunia katika uzani huo Floyd Mayweather. Akizungumza na waandishi wa habari Khan amesema anaamini kwamba amepata fursa ya kupambana na Bondia Mayweather baada ya ushindi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako