• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misaada ya China kwa nchi za nje ni wazi na inatoa kipaumbele kwa maisha ya watu

    (GMT+08:00) 2014-12-17 10:48:50

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Shen Danyang, amesema misaada inayotolewa na China kwa nchi za nje inazingatia uwazi na kusimamiwa kisayansi, ambapo miradi inayohusiana moja kwa moja na maisha ya watu inapewa kipaumbele.

    Msemaji huyo amesema hayo kwa kujibu ripoti iliyotolewa hivi karibuni na shirika moja la Marekani ikisema fedha nyingi za misaada ya China kwa nchi za nje zimetumika katika maskani ya viongozi wa nchi zinazopokea misaada hiyo.

    Bw. Shen Danyang amekanusha ripoti hiyo akisema, lengo la misaada ya China ni kuboresha maisha ya watu, kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii, na kuongeza uwezo wa kujiendeleza wa nchi zinazosaidiwa. Amesema kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2012, asilimia 80 ya fedha za misaada zilitolewa katika upunguzaji wa umaskini, elimu, afya, michezo, utamaduni, mawasiliano na sekta nyingine zinazohusiana maisha ya watu na miundo mbinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako