Klabu ya Yanga ya Tanzania imemtimua kocha Marcio Maximo baada ya timu hiyo kunyukwa magoli 2-0 kwenye mechi ya Mtani Jembe iliyogaragazwa jumamosi katika uwanja wa taifa Dar es Salaam.Wachezaji wa Yanga walionekana wakidondokwa na machozi wakati Maximo alipokuwa akiwaaga rasmi kwenye mazoezi katika uwanja wa Sekondari ya Loyola jijini Dar es Salaam. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa klabu hiyo walielezea kutoridhishwa kwao na uamuzi wa uongozi wa klabu yao kumfuta kazi kocha wao na mshambuliaji Hamis Kiiza kutoka Uganda.Maximo amewapa moyo wachezaji hao na kuwataka wajitume kwa kuwa ni wachezaji wazuri na timu ni nzuri na kuwataka kuongeza bidii ili wafike mbali. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameunga mkono uamuzi wa kumtimua Maximo wakisema timu haikuwa na uwezo wa kupambana na timu pinzani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |