• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyota wa zamani wa Arsenal Thierry Henry astaafu rasmi kucheza soka

    (GMT+08:00) 2014-12-17 15:22:41

    Nyota wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry hatimaye ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka. Nyota huyu alietwaa kombe la dunia mwaka 1998 akiwa na timu ya Ufaransa alijiondoa kwenye klabu ya New York Red Bulls mapema mwezi huu na kuzua tetesi kuwa angejiunga na klabu nyingine kubwa barani ulaya.Akitoa tangazo hilo, Henry amewashukuru mashabiki, wachezaji wenzake katika timu zote ambazo amechezea kwa kumwezesha kutimiza ndoto yake. Henry alianza kuwika kwenye soka ya kimataifa akianzia na klabu za Monaco, Juventus kabla ya kutua Arsenal alikocheza kwa mafanikio makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako