• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Afrika kutoa fedha kwa ajii ya ukarabati wa bwawa linalomilikiwa na Zambia na Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2014-12-18 10:12:47

    Benki ya maendeleo ya Afrika imekubali kutoa dola milioni 75 za kimarekani kwa ajili ya ukarabati wa bwawa la Kariba linalomilikiwa na Zambia na Zimbabwe.

    Uamuzi huo umeongeza jumla ya fedha zinazotolewa na wafadhili zifikie dola za kimarekani milioni 175 kufuatia Benki ya dunia na serikali ya Uswisi kuidhinisha dola milioni 75 na milioni 25 za kimarekani kwa ajili ya ukarabati wa bwawa la Kariba.

    Bwawa hilo ambalo ni kubwa kabisa barani Afrika, liko katika hatari ya kubomoka kama hatua za dharura hazitachukuliwa ndani ya miaka mitatu ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako