• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya  kandanda ya Afrika mashariki na kati CECAFA kutofanyika mwaka huu

    (GMT+08:00) 2014-12-18 14:21:31
    Michuano ya kandanda ya Afrika mashariki na kati CECAFA haitafanyika mwaka huu kutokana na kukosa mahali pa kuiandaa michezezo hiyo.

    Hata hivyo Rais wa CECAFA Leodegar Tenga amesema kuendelea kuongezeka kwa gharama ya kuandaa michuano hiyo ndio sababu kuu ya kutokuwa na mashindano hayo mwaka huu.

    Amesema sasa wanajadili njia za kupunguza gharama za kuandaa michezo hiyo inayojumuisha timu 12.

    Rais huyo alisema pia pesa ambazo CECAFA imepata hadi sasa hazitoshi lakini mjadala unaendelea jinsi ya kuwa na mipango bora ili miaka ijayo michezo hiyo ifanyike.

    Ethiopia ilijiondoa kutoka uandaaji wa michezo hiyo na hakuna nchi nyingine iliyoonyesha nia ya kuiandaa jambo ambalo wadau wanalitaja kama pigo kubwa kwa kdandanda kwenye kanda hiyo ya Afrika mashariki na kati.

    Inagharimu tarkriban dola 600, 000 kuandaa shindano la CECAFA ambalo hufanyika ndani ya wiki mbili likijumuisha nchi za Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, South Sudan, Sudan, Tanzania, Uganda, Zambia na Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako