Mkongwe wa soka Henry Thierry ametangaza amestaafu baada ya kuchezea kwa muda mrefu vilabu mbalimbali kama vile Arsenal na Barcelona. Amesema staa huyo kwamba amefurahia kuchezea timu kubwa na sasa anajiunga na kituo cha televisheni kuwa mchamnbuzi wa michezo.
Henry ni mfungaji bora anayeongoza nafasi ya pili katika kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA), na mchezaji bora nchini Ufaransa mwaka 1997. Henry aliichezea pia klabu ya Juventus kwa kipindi cha miezi saba na kupelekea ushindi wa klabu hiyo wa Kombe la Intertoto.
Na sio hayo tu ya kujiuzulu kwa Henry Thierry mbali pia kule ujerumani mshambulizi wa kimataifa Mike Hanke pia naye amesema atang'atukla kutoka uwanjani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema sasa hana hamu tena ya kucheza kandanda baada ya kung'ara kwenye bundesliga kwa karibu miaka 12.
Hanke mara ya mwisho aliichezea timu ya Guizhou Renhe nchini China lakini baada ya mechi 12 alifunga bao moja tu na hivyo akaamua kusitisha mkataba wake mwezi Oktoba.
Hata hivyo mairi huyo wa Ujerumani aliwahi kuchezea klabu za Wolfsburg, Hannover, Freiburg na kwa jumla amefunga mabao 54 katika mechi 284.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |