Serikali ya Kenya na kamati ya olimpiki zitaandaa warsha ya siku moja mjini Nairobi leo kujadili swala la matumzi ya dawa za kutitimua misuli miongoni mwa wanariadha.
Huku kukiwa na visa 18 vilivyoripotiwa ndani ya miaka 2 iliopita Kenya imeonekana kuwa moja wepo wa nchi ambayo wanariadha wake hutumia sana dawa hizo kama vile nchi za Marekani Russia na Jamaica.
Mwenyekiti wa kamati ya olimpiki nchini Kenya Kipchoge Keino amelitaja swala hilo kuwa kubwa na sasa umefika wakati wa kulijadili na kutafuta sukuhulu.
Alsema kuwepo na visa vya matumizi ya dawa kunaharibu sifa ya wanaridha wa Kenya ambao wanatambulika kote duniani kwa umairi wao kwenye mashindano makubwa kama vile olimpiki.
Warsha hii inafanyika siku kadhaa baada ya rais wa riadha nchini Kenya Isaiah Kiplagat, kukataa kutoa ushaidi na habari kuhusu matumizi ya dawa kwa jopo kazi la kupambana na dawa hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |