Timu ya taifa ya soka ya Algeria imekuwa ya kwanza kutangaza kikosi chake cha wachezaji 23 kitakachoshiriki katika mechi za mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Equitorial Guinea.
Kocha Christian Gourcuff amemtaja kiungo wa kati wa klabu ya Newcastle United ya Uingereza, Mehdi Abeid.
Abeid mweye umri wa miaka 22 na ambaye hajawahi kuichezea timu ya taifa, ni miongoni mwa wachezaji watano wapya waliopata nafasi katika kikosi hicho.
Algeria ipo katika kundi la C pamoja na Ghana, Senegal na Afrika Kusini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |