• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kushirikisha jamii kwenye uhifadhi nchini Kenya kwatambuliwa kimataifa

    (GMT+08:00) 2014-12-18 15:42:34

    Kenya ni miongoni mwa nchi nane kote duniani ambazo zimetunikiwa tuzo la Green list ambalo linatolewa na shirikisho la kimataifa la kuhifadhi mazingira na mali asili IUCN. Kenya pia imekuwa ya kwanza barani Afrika kupata tuzo hilo lililotolewa Mjini Sydney Australia. Ronald Mutie anaripoti.

    Nchi nyingine ambazo zimepata tuzo hilo ni pamoja na Australia, Korea Kusini, China, Italia, Ufaransa, Hispania, na Colombia. Nchini Kenya mashirkka mawili Lewa Consercvancy na Ol Pajeta ndio yalipata tuzo hilo. Bi Ruwaydah Abdul Rahaman ni meneja wa mauhusiano ya wafadhili kwenye hifadhi ya Lewa.

    "Lewa ilitambuliwa sana sana katika ubora wake wa kuhifadhi wanyama pamoja na mipango mbalimbali ya maendeleo ya jamiii katika elimu, afya, uwezeshaji wa wanawake na vijana na kubadilisha maisha"

    Jamii nyingi za eneo la Lewa ni wafugaji na wakulima. Kuendelea kuongezeka kwa idadi ya watu na mahitaji ya chakula na maji kunamanisha kupungua kwa makaazi ya wanyama pori. Awali wanyama kwenye eneo la Lewa walikuwa kwenye hatari. Wakaazi hawakupata fedha za kutosha kutoka kwa shughuli za kilimo na ufugaji na hivyo mara kwa mara waliwinda kuuza bidhaa za wanyama pori. Kulikuwa na mwingiliano wa binadamu na wanyama pori lakini walioumia zaidi ni wanyama. Hiyo ilipelekea hifadhi nyingi nchini Kenya kama Lewa kufikiria upya kuhusu uhifadhi.

    "Tunapenda kuona jambo la kwanza, sio kuhifadhi wanyama peke yake lakini kuendeleza maisha ya jamii ambao tunafanya kazi nao. Inaturuhusu zaidi kutangza mambo ya jamii kuhifadhi wanyama pori kwa hivyo tunahifadhi wanyama na jamii inayoishi karibi na hili eneo "

    [Daktari akimhudumia mkaazi wa eneo la Lewa. Kushirikisha jamii kwa njia ya kuwapatia msaada utokanao na mapato ya watalii hifadhi ya Lewa imetambuliwa na kupata tuzo la Green list ambalo linatolewa na shirikisho la kimataifa la kuhifadhi mazingira na mali asili IUCN.]

    [Bi Ruwaydah Abdul Rahaman ni meneja wa mauhusiano ya wafadhili kwenye hifadhi ya Lewa. Anasema asilimia 70% ya watu ambao wanafanya kazi hapa ni jamii za karibu na hiyo inasaidia kupunguza kuingia kwa watu kutoka nje ambao wanaweza kuuwa wanyama.]

    Licha ya kwamba uwindaji wa wanyama pori umekidhiri sana kwenye hifadhi za wanyama barani Afrika, mwaka huu hifadhi ya lewa haijakuwa na kisa chochote cha kuuwawa kwa kifaru ambao huwindwa sana kwa ajili ya pembe zake. Lakini haijakuwa rahisi kupunguza uwindaji haramu na jamii imetekelza wajibu muhimu, anasema Rahaman.

    "Asilimia 70% ya watu ambao wanafanya kazi hapa ni jamii za karibu kwa hivyo tunapunguza kuingia kwa watu kutoka nje ambao wanaweza kuuwa wanyama"

    Hata hivyo Rahman anasema kuendelea kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za wanyampori tayari ni jambo la kutia hofu na matumaini yake ni kwamba suluhu litapatikana.

    [Wanafunzi katika shule ya Rugusu ambayo imejengwa kwa ufadhili kwa ufadhili wa hifaddi ya Lewa.  Tangu ianze, Lewa imejenga shule ishirini katika jamii na inafadhili miradi ya shule kama vile mabweni, maktaba, vitabu na waalimu. Wamejenga pia shule sita za watu wazima ambao baada ya masomo wanapewa mikopo midogo ili kuwawezesha kuanza biashara]

    [Mradi wa kutoa vifaa vya kawi ya jua.(Solar). Kawi endelevu kama hii inasaida wanafunzi kuendelea na masomo hata usiku na wakati huo huo ni njia moja ya kutunza mazingira ambayo ni muhimu kwa mfumo wa ikolojia.]

    Zaidi ya kilomita 120 hivi kutoka Lewa ni hifadhi ya Ol Pajeta ambayo pia imetunukiwa tuzo la Green List. Kama vile lewa Ol pajeta pia ina mpango maalum wa kushirikkisha jamii kwenye uhifadhi. Juhudi za kushirikisha jamii hapa pia zimezaa matunda kama anavyoeleza Samuel Mutisya mmoja wa wasimamizi kwenye hifadhi hiyo.

    "Hao pia wamekuja kujua kwamba uwindaji haramu unawaathiri na sasa wanatupatia ujumbe kuhusu njama za uwindaji haramu ambazo ziko kwenye jamii na hiyo inatusaidia kusimamisha njama kama hizo ama kujitayarisha ili hao wahalifu wakija wasipate nafasi ya kuingia. Kwa hivyo kuishi pamoja kwa utangamano imekuwa faida kwetu sisi na kwa hao pia kwa sababu zile pesa ambazo tunakusanya kupitia mapato ya kitalii tunazirudisha kwenye jamii ili wanufaike"

    Nayo jamii inayoishi karibu na lewa pia imefaidika kwa kupata miradi mbali mbali ya maendeleo inayofadhiliwa na hifadhi hiyo. Miradi hiyo inawasaidia kujikinga na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kupata maarifa ya kufanya biashara. Bi Abdulrahaman anasema.

    "Lewa tangu ianze imejenga shule ishirini katika jamii za hapa na tunaendelea kufadhili miradi ya shule kama vile mabweni, maktaba, vitabu na waalimu. Tuna shule pia sita za watu wazima na tunafundisha watu ambao hawakuweza kwenda shuleni zamani. Na baada ya masomo tunawapea mikopo midogo ili kuwawezesha kuanza biashara. Na pia tuna miradi ya maji kwa jamii kama kumi hivi kwa sababu eneo hili huwa lina ukame wakati mwingine"

    Kwa kuwa jamii ya eneo la Lewa inajumuisha wakulima na wafugaji, hifadhi hii imetenga maeneo kadhaa ili watu walishe mifugo wao. Hii pia ina manufaa kwani inalainisha na kurotubisha udongo kwenye hifadhi. Hifadhi ya Ol pajeta pia ina mradi maalum wa kuwasaidia wakulima.

    "Ukuzaji wa kama mboga na mimea mingine. Tunawapatia pia maarifa ya kufanya kilimio kwenye maeneo ambayo yanapata mvua kidogo ili wapate chakula cha kutosha na hata kuuza"

    Huku mahitaji ya ardhi na raslimali za maji ikiendelea kuongezeka sawa na kupanda kwa bei ya bidhaa kama vile pembe za ndovu, inasalia jukumu la wahifadhi kushirikisha jamii kwenye uhifadhi wa wanyama pori ili idadi ya wanyama iendelee kukua sio tu kwa manufaa ya mapato ya utalii mbali pia na jamii yenyewe.

    [Kwa kuwa jamii ya eneo la Lewa inajumuisha wakulima na wafugaji, hifadhi hii imetenga maeneo kadhaa ili watu walishe mifugo wao. Hii pia ina manufaa kwani inalainisha na kurotubisha udongo kwenye hifadhi. ]

    [Ujenzi wa Shule ya Irura ambayo inafaidi jamii za karibu na hifadhi ya Ol pajeta. Hifadhi hii ilipata tuzo la Green list ambalo linatolewa na shirikisho la kimataifa la kuhifadhi mazingira na mali asili IUCN. Mojawepo wa sababu za kupata tuzo hilo ni kushirikisha jamii kwenye shughuli zake za kuhifadhi wanyama]

    [Wakaaazi wa karibu na eneo la Ol pajeta wamtazama (sokwe) Chimpanzee. Mara kwa mara wanapata fursa ya kuingia bila malipo kwenye hifadhi hiyo kujionea mahadhari na wanyama. Hii inawasaida kujenga mawazo yao kuhusu umuhimu wa kuhifadhi wanyama pori. Sehemu ya mapato kutoka kwa watalii wanaokuja hapa hutumika kufadhili miradi ya maendeleo kwenye jamii.]

    [Mbali na kutoa huduma za kusaidia kilimo cha mboga hifadhi ya Ol Pajeta pia inatoa huduma za nyanjani kwa wafugaji wa ngo'ombe wa maziwa kama hawa. Wafugaji pia wanakubaliwa kulisha mifugo wao kwenye maeneo yaliotengwa haswa wakati wa kiangazi.]

    [Mradi wa kunyunyiza maji kwa mimea kwa kutumia teknolojia isiyohitaji maji mengi. Mradi huu wa nyumba kitalu unafadhiliwa na hifadhi ya Ol pajeta kama mojawepo wa juhudi jamii jirani na hifadhi hiyo ili kuwawezesha kujitosheleza chakula. ]

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako