• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nguvu mpya ya umoja wa mataifa huenda ikasaidia kumaliza upashaji tohara kwa wanawake.

    (GMT+08:00) 2014-12-19 10:18:16

    Takwimu za shirika la Umoja wa mataifa la kuwahudumia watoto la Unicef zinaonyesha kwamba zaidi ya wasichana milioni 30 wako katika hatari ya kukeketwa katika kipindi cha chini ya miaka kumi ijayo.

    Licha ya kwamba kitendo kinapingwa na nchi nyingi kupitia kwa sharia na wanaharakti bado kimekuwa vikifanyika.

    Lakini hivi karibuni harakati dhidi ya kuwatairi wanawake zilipata nguvu mpya baada ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon kuzindua kapmeni ya kumaliza tamaduni hiyo.

    Ronald mutie anaripoti

    Mjadala kuhusu upashaji tohara kwa wanawake nchini Kenya umekuwepo kwa muda mrefu.

    Wanaharakati wa kitaifa katika maeneo yalioathiriiwa na tohara wameendeleza kampeni za kupinga tamaduni hiyo ambayo pia iko kwenye nchi nyingi barani Afrika na sehemu za mashariki ya Kati.

    Lakini kampeni zao mara kwa mara zimekumbana na upinzani mkali kutoka kwa jamii.

    "Waswahili husema mwacha mila ni mtumwa, kwa nini mnataka kunifanya niwe kama mtumwa? Waniachishe mila yangu? Kikwetu sisi tunasema kijufungua kwa msichana ambaye hajafanywa tohara ndio ngumu kuzaa na kwetu sisi tukiwa tumetahiriwa ndio rahisi"

    Ukiwa ni utamaduni unaopelekea hata na kuwepo kwa ndoa za mapema, umekuwa na athari kubwa kwa wanawake haswa walioko kwenye maeneo yasiofikiwa kwa haraka na huduma za serikali ama mashirika.

    Lakini mwishoni mwa mwezi oktoba mjini Naiorbi juhudi za kupambana na tohara kwa wanawake zilipata nguvu mpya yenye ushawishi.

    Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon alizindua kampeni ya kimataifa dhidi ya tohara kwa wanawake.

    "Upashaji tohara kwa wasichana na wanawake lazima ukomeshwe kwenye kizazi hiki…wavulana na wanaume pia wanafaa kuhimizwa kuunga mkono vita dhidi ya upashaji tohara kwa wanawake na pia wanafaa kupongezwa wanapofanya hivyo. Habari zuri ni kwamba jamii nchini Kenya na kote barani Afrika na duniani zimekubali kusitisha upashaji tohara kwa wanawake"

    Kampeni hiyo ya umoja wa mataifa inafuatia kupitshwa kwa maazimio ya baraza kuu la umoja huo mwaka wa 2012 ya kuondoa kabisa upashaji tohara kwa wanawake.

    Lakini hata wakati Ban akianzisha kampeni hiyo tohara kwa wanawake tayari imekithiri kwenye jamiii za afrika na imeleta athari nyingi kwao.

    Dkt Francis Were ni mtaalam wa gainakolojia kutoka Kenya.

    "Mwanamke aliyetairiwa wakati akipata mimba anakuwa na shida wakati wa kujifungua na pia motto anapotoka mama huenda akavuja damu kwa wingi na hiyo inaweza kuhatarisha maisha yake. Hatari ilioko kwa mfano Yule mpasha toara hutumia vifaa butu na ambavyo havijasafishwa vizuri na hiyo inaweza kusababisha maradhi kama vile pepopunda, hepatitis na wengine wanaweza kuambukizwa HIV"

    Taakwimu za shirika la afya duniani zinaonyesha kwamba zaidi ya wanawake milioni 125 wamepashwa tohara katika nchi 29 za Afrika na mshariki ya kati.

    Shirika hilo linataja upashaji tohara kwa wanawake kama ukiukaji wa haki zao.

    Baadhi ya serikali za zimejitahidi kuunda sharia ya kupambana na tamaduni hiyo ili kuokoa mamilioni ya wasichana na wanawake.

    Nchini Kenya kwa mfano, mwaka wa 2011 serikali ya Kenya ilipitisha mswada kuifanya tohara kwa wanawake kuwa kinyume cha sheria na yeyote atakayepatikana akishiriki kitendo hicho atahukumiwa kifungo kisichopungua miaka 3 gerezani faini na hata kufungwa maisha iwapo aliyetairiwa atafariki.

    Lakini hata hivyo tamaduni hiyo bado inaendelezwa kwenye usiri mkubwa na mara nyingine ikidaiwa kusimamiwa na wazee wa vijiji ama machifu.

    Kuzinduliwa kwa kampeni hii ya kimataifa kutasaidia kupunguza upashaji toara aghalabu kwa wanawake, lakini katika siku za baadaye Ban Ki- moon anasema jamii itakuwa na wajibu muhimu wa kupingana na utamaduni huo.

    Pia sio nchi zote ambazo zimepitisha sharia ya kupinga tohara kwa wanawake.

    Lakini kupitia kwa kampeni za wanahakari kama vile shirika la Kakenya wasichana wengi wanaokolewa kutoka kwa utamaduni huo na kuwawezesha kuendelea na masomo.

    Bi. Kakenya Ntaiya ni mwanzilishi wa shirika hilo.

    "Sio hadithi tu mbali ni maisha ya wasichana, ndoto zao, matumaini yao, na maisha yao yanaangamizwa…..Nawaambia hivyo kwa sababu huu sio utamaduni wala desturi lakini ni ukiukaji wa haki za binadamu, ukiukaji wa haki za watoto ambao hata hawajui mustakhabali wao…basi kwa nini tunaacha jambo hili kuendelea."  

    Licha ya kuwa utafiti wa kiafya nchini Kenya unaonyesha kwamba upashaji tohara umepungua kwa wanawake wa kati ya umri wa miakla 15 na 49 kutoka 37 mwaka wa 1998 hadi asilimia 27 mwaka wa 2008 bado asilimia ya wanawake wanaotairiwa imesalia kuwa juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako