Winga matata wa Manchester United, Angel Di Maria alimpiku straika hatari wa Barcelona, Lionel Messi na kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Argentina.
Di Maria ambaye anauguza majeraha, alizoa kura za kutosha zilizopigwa na waandishi wa spoti wa taifa hilo na kuibuka mshindi mbele ya Messi aliyemaliza wa pili.
Winga huyo aliyejiunga na United mapema msimu huu kwa dau la dola milioni 93 za kimarekani alitangazwa mshindi wa tuzo hilo la Olimpa de Plata Jumanne usiku jijini Buenos Aires.
Mchango wake mzuri wa kuisadia klabu yake ya zamani Real Madrid kushinda taji lao la 10 la Ueafa, 'La Decima', pamoja na kuifikisha Argentina kwenye fainali ya kombe la dunia na vile vile mwanzo wake wa kuridhisha kwenye ligi ya Uingereza, ndivyo vigezo viliyovyompelekea kutangazwa mshindi.
Kwa upande wa Messi, kile kinachoonekana kumwangusha ni kukosa kuisaidia Barcelona kufika mbali kwenye dimba la klabu bingwa Ulaya pamoja na kupoteza taji lao la ligi kuu lililotwaliwa na mabingwa watetezi Atletico Madrid.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |