Mchezaji wa Ragbi anayeongoza kwa wingi wa pointi duniani Daniel Carter atajiunga na klabu ya Racing Metro ya Ufaransa kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Cater mwenye umri wa miaka 32 sasa atakuwa ndiye mchezaji wa ragbi anayelipwa pesa nyingi zaidi akiwa atatia kibindoni dola milioni 2 kwa mwaka.
Hii ni mara ya pili kwa Cater kujiunga na klabu ya ufaranza awali mwaka wa 2008 alikuwa amesajiliwa kwa kandarasi ya miezi saba na klabu ya Perpignan lakini alicheza mechi 5 tu na kupata jeraha.
Mchezaji huyo wa New zealand anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo mpya mwaka ujao na kuendelea kucheza hadi mwaka wa 2018.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |