• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baloteli atozwa faini na kufungiwa mechi moja.

    (GMT+08:00) 2014-12-19 14:26:18

    mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli amepata adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja na Chama cha Soka nchini Uingereza, ikiwa ni kutokana na kile mchezaji huyo alichokiandika katika mitandao ya habari ya kijamii.

    Kutokana na adhabu sasa nyota huyo wa Italia,hatakuwepo uwanjani wakati timu yake ya Liverpool itakapoikaribisha Arsenal Jumapili, katika michezo ya ligi kuu ya Uingereza.

    Na mbali na kufungiwa kucheza mechi hiyo pia Baloteli mwenye umri wa miaka 24 amepigwa faini ya pauni £25,000 na kutakiwa kuhudhuria kozi ya elimu.

    Inadaiwa kuwa Mchezaji huyo alirudia kutuma picha ya mchezo wa kompyuta yenye kibonzo cha Super Mario katika mtandao wa Instagram ambacho kilikuwa na maneno "ruka kama mtu mweusi na kusanya sarafu kama myahudi."

    Baadaye alituma ujumbe wa tweeter akikanusha kuwa ujumbe huo ulikuwa na makosa, kabla ya kuomba radhi.

    Baada ya kujua adhabu yake, aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook kwamba uamuzi wa FA "umeonyesha wazi" kwamba ujumbe wake ulikuwa "makosa".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako