Wachezaji kandanda wameanza kuwasili nchini Somalia kwa ligi ya soka katika nchi hiyo iliokuwa kwa kipindi kirefu cha vita. Mashindano ya mwaka huu yatashuhudia idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni.
Kuongezeka kwa hali ya utulivu katika mji mkuu, Mogadishu kumevutia kiasi cha wachezaji ishirini wa soka kutoka Nigeria, Kenya, Uganda na nchi nyingine za Kiafrika.
Pia kuna kocha wa kigeni John Maura ambaye anakuwa kocha wa kwanza kuongoza klabu kubwa nchini Somalia kwa karibu miaka thelathini.
Kocha huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kufundisha timu ya Banadir Sports Club, ambao ni mabingwa wa ligi ya Somalia.
Kwa jumla ligi ya taifa mwaka huu inajumuisha timu 10 ikilinganishwa na timu 8 za mwaka jana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |